KAZI ZIPO ENTERPRISES ni jukwaa huru linalo toa fursa mbalimbali kwa vijana wanao tafuta kazi (Ajira rasmi pamoja na ajira zisizo rasmi yaani vibarua vya kila aina.
Lakini pia jukwaa hili linawapa nafasi waajiri wanao tafuta wafanya kazi kuweka matangazo ya kazi, ili waweze kupata wafanya kazi kwa njia nyepesi na ya haraka.
Pamoja na hayo, jukwaa hili pia linawapa fursa wafanya biashara wote, kutangaza biashara zao, tuna amini uwezekano wa wafanya biashara kuongeza idadi ya wateja ni mkubwa sana maana jukwaa hili linatembelewa na idadi kubwa sana ya watu.
Vilevile jukwaa hili halija wasahau mafundi. Kama wewe ni fundi wa kutengeneza kitu chochote, jukwaa hili pia litakufaa sana kuweza kujitangaza na kupata tenda mbalimbali kwenye kazi yako.
Hivyo tunafuraha kuona kuwa tunafanyika mwarobaini kwa kila tatizo hususani mambo ya kazi na ajira pamoja na biashara.
Tumesajiriwa kwa mujibu wa sheria na tunafanya kazi kisheria.
Jukwaa hili kazi yake kubwa ni kuwakutanisha watu (to link clients) Hivyo kama kati yenu mmoja hata ridhika na huduma ya mwenzake ni uamuzi wake kuachana nayo ili asiingie kwenye hatari ambayo hakuitegemea.
KAZI ZIPO ENTERPRISES haitahusika na makubaliano ya aina yeyote yatakayo fanywa baina ya MTEJA NA MUUZAJI, au BAINA YA MWAJIRI NA MWAJIRIWA. (Mtafuta wafanya kazi na mtafuta kazi).
ZINGATIA: KILA TANGAZO LA KAZI UTAKALO LIONA KATIKA JUKWAA HILI LINA MAWASILIANO YA MTOA TANGAZO/KAZI, HIVYO MAKUBALIANO YA HIYO KAZI UNAYO TAKA KUIOMBA MTAYAFANYA WENYEWE PASIPO KUINGILIWA NA KAZI ZIPO ENTERPRISES.